tmoja2

Aliyeandika jumbe za uchochezi Facebook kuhusu Dkt Shien na Mwamunyange akamatwa Arusha

117
0
Share:
Share this
Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha linamshikilia Mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru aliyejulikana kwa jina la Harold Mmbando (23) kwa kosa la kutoa taarifa za uchochezi dhidi ya Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein na Mkuu wa majeshi Jenerali Davis Mwamunyange.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo alisema kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo Mei 17 mwaka huu saa 09:00 asubuhi .
Ameeleza kuwa mtuhumiwa alaindika haya katika mtandao wa Facebook “Mwamunyange pindua nchi haiwezekani wote wawe nje halafu hakuna aliyepewa mamlaka ya kukalia kile kiti.”
Aidha mtuhumiwa aliandika ujumbe mwingine kuwa ,”Dkt Shein akiuawa kama Karume sitashangaa wala kushtuka naomba Mungu mauaji ya kisiasa yaliyotokea Zanzibar yawe kwa viongozi wa kisasa hasa watawala na sio wananchi wa kawaida”.
Kamanda wa Polisi alisema kuwa, ni vyema wananchi wakatumia mitandao kwa njia iyakayolisaidia taifa badala ya kutumia kusambaza jumbe za matusi au uchochezi kwani watajikutaka katika mazingira magumu.

Comments

error: Content is protected !!