Atozwa faini na Polisi kwa kosa la kufunga taa zenye mwanga mkali kwenye gari

531
0
Share:
Share this
CMTL Group

Jeshi la Polisi linaendelea na msako wa kuwakamata na kuwachukulia hatua madereva wote waliofunga taa zenye mwanga mkali (sports light) kwenye magari yao.

Jeshi la Polisi lilitoa tahadhari awali kuwa ni marufuku kufunga taa hizo kwenye magari kwa sababu zimekuwa chanzo cha ajali barabarani hasa nyakati za usiku. Mwanga wa taa hizi ukimmulika dereva mwingine humsababishia kushindwa kuona kwa muda mfupi na hivyo kupelekea hatari kwa dereva huyo na watumiaji wengine wa barabara.

Dereva Mohammed Suleiman anayefanya safari zake kati ya Moshi na Shinyanga Mjini amekamatwa na Polisi Moshi kisha kutozwa faini ya TZS 30,000 kwa kosa la kufunga taa hizo

whatsapp-image-2017-01-10-at-1-15-59-pm

Madereva wengi wanaofunga taa hizi hudai kuwa wanazitumia panapokuwa na ukungu mkali kuweza kuona mbele na pia wanapopita kwenye mapori. Lakini wapo baadhi ya madereva ambao huzitumia hata wanapokuwa katika ya miji.

Comments

error: Content is protected !!