tmoja2

Bodi ya Mikopo yaja na mbinu nyingine ya kukusanya madeni kwa wadaiwa sugu

216
0
Share:
Share this
tmoja2

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Abdul Razaq Badru amesema kuwa kuanzia Januari mwakani bodi hiyo itachapisha majina ya wadaiwa sugu kwenye mitandao na vyombo vya habari ili jamii iwafahamu wale wanaokwamisha juhudi za kusaidia wengine.

Abdul Badru ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu urejshwaji wa mikopo na wanafunzi ambapo alisema kuwa mwanzoni waliweka majina pekee lakini sasa hivi wataweka na picha ili jamii ikiwaona iwafahamu.

Aidha alisema kuwa tangu walipotangaza majina ya wadaiwa sugu, takribani wadaiwa 42, 700 wamejitokeza ambapo baadhi wamelipa madeni yao yote huku wengine wakilipa sehemu ya madeni yao.

Akizungumzia muda ambapo mwanafunzi aliyenufaika na mkopo anapaswa kuanza kurejesha, Abdul Badru alisema kuwa, mnufaikaji wa mikopo anatakiwa kwa mujibu wa sheria kuanza kurejesha  mkopo wake baada ya miaka miwili tangu amalize chuo. Lakini alisema mtu anaweza kuanza kabla ya muda huo kama amejiajiri au alipata ajira mapema.

 

Comments

error: Content is protected !!