tmoja2

Bodi ya Mikopo: Zoezi la kufanya uhakiki kwa wanufaika; Fahamu kitakachowakuta watakaopungukiwa na vigezo

265
0
Share:
Share this
tmoja2

Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya Juu leo imetoa ufafanuzi wa masuala mbali mbali kuhusu zoezi la utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wapya na wale wanaoendelea, huku ikitangaza kuanza kwa zoezi la uhakiki wa wanufaika wa mikopo inayotolewa na bodi

Mkurugenzi Mtendaji wa bodi hiyo Bw. Abdul-Razaq Badru amesema hayo katika mkutano wake na wanahabari jijini Dar es Salaam leo na kwamba zoezi hilo litadumu kwa kipindi cha mwezi mmoja ambapo wale watakaopungukiwa na vigezo hawataendelea kupatiwa mikopo.

Kwa mujibu wa Bw. Badru, zoezi hilo litasaidia kuwa na taarifa kamili za kila aliyepata mkopo, zoezi litakalopunguza urasimu pamoja na manung’uniko ya baadhi ya watu kutopata mikopo.

Aidha, amesema uhakiki huo utaisaidia serikali kuwa na usimamizi bora wa pesa inazozitoa kwa wanafunzi wa elimu ya juu nchini na kwamba kila mwanachuo anapaswa kujaza fomu maalum zitakazopatikana kwenye tovuti ya bodi hiyo.

Awali katika maelezo yake, Mkurugenzi Mtendaji huyo wa Bodi ya Mikopo amesema jumla ya fedha za Tanzania shilingi bilioni 483 zimetengwa kwa ajili ya kuwapatia mikopo wanafunzi kwa mwaka huu wa fedha na kwamba kati ya hizo, shilingi bilioni 56 zitatokana na makusanyo kutoka kwa wadaiwa waliokopeshwa na bodi hiyo miaka ya nyuma.

 -EATV

Comments

error: Content is protected !!