Diamond atajwa kutumbuiza katika sherehe nyingine kubwa Afrika Januari 14

562
0
Share:
Share this
CMTL Group

Mwanamuziki Naseeb Abdul maarufu Diamond Platnumz kutoka nchini Tanzania ametajwa kutumbuiza katika tamasha lingine kubwa barani Afrika ikiwa ni siku chache tu tangu alipotumbuiza katika sherehe za utoaji tuzo za Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Januari 14 mwaka huu, Diamond atakuwa jukwaani nchini Gabon akitumbuiza katika sherehe za ufunguzi wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2017.

Kupitia ukurasa wao wa Twitter, waandaji wa michuano hiyo wameandika “Next week #AFCON2017 Gabon opening ceremony Diamond Platnumz.”

whatsapp-image-2017-01-09-at-6-15-45-pm

Diamond amewataka mashabiki wake na wapenzi wa muziki nchini Gabon kukaa tayari kwani anakuja kuweka historia ya muziki.

Michuano ya AFCON 2017 inatarajiwa kuanza Januari 14 kwa michezo miwili ambapo wenyeji Gabon watatupa karata yao ya kwanza dhidi ya Guinea-Bissau mchezo utakaoanza saa 1:00 jioni (saa za Afrika Mashariki) na mchezo mwingine ni Burkina Faso dhidi ya Cameroon saa 4:00 usiku (saa za Afrika Mashariki).

Mabingwa watetezi wa kombe hili, Ivory Coast wametengewa kitita cha TZS bilioni 12.9 ili waweze kulitwaa tena kombe hilo. Mara ya mwisho mwaka 2015 walilitwaa kombe hilo baada ya kuifunga Ghana kwa penati 9-8.

Comments

error: Content is protected !!