tmoja2

Habari 6 kubwa Tanzania leo Juni 25

153
0
Share:
Share this
  1. Uzinduzi wa mpango wa kuboresha usalama wa jamii biafra

tmoja2

Mgeni rasmi katika shughuli hizi za Uzinduzi leo alikua ni Rais Dkt John Magufuli ambapo alizindua Mpango wa kuboresha usalama wa jamii na mali zao, ambao una dhamira ya kupunguza uhalifu na vile vile aliagiza jeshi hilo kuwahi kushughulikia majambazi kabla ya wenyewe kushughulikiwa na majambazi hao.  Awali Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Ernest Man alisema mpango huo unalenga Kuboresha mbinu za kupambana na wahalifu na majambazi, moja kwa kuwa na vituo vya polisi vya kuhamahama kufikia sehemu ambazo hazina vituo vya polisi na uhalifu umekithiri, mbili kutumia mfumo wa kisasa wa GPS katika doria za jeshi hilo, tatu kuwa na Call Center ambapo watapata taarifa moja kwa moja kutoka kwenye matukio na kuyatatua ndani ya dakika chache hii yote ikiwa na nia ya kuongeza ubora wa huduma katika vituo vya polisi ambapo polisi watakuwa wanatatua na kusikiliza kero za wananchi kwa haraka zaidi na kwa muda mfupi sana.

2. Zaidi ya wanafunzi 90,200 kutinga kidato cha 5 na vyuo.

Jumla ya wanafunzi 90,248 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi mwaka 2016 ambapo kati yao wasichana ni 28,911 na wavulana 36,050. Hata hivyo, jumla ya wanafunzi 24,258 sawa na asilimia 27.2 wenye sifa wamekosa nafasi za kujiunga na kidato cha tano kutokana na ufinyu wa nafasi za shule hizo. Matokeo ya uchaguzi wa wanafunzi hao yalitangazwa jana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene (pichani) na kubainisha kuwa jumla ya shule 326 zikiwemo mpya 47 zimepangiwa wanafunzi wa kidato cha tano- HABARI LEO

  1. Sheria kuwabana Mafisadi yapita.

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, jana lilipitisha kwa kauli moja Sheria ya Marekebisho Mbalimnbali, ambayo pamoja na mambo mengine, yamempa Jaji Mkuu mamlaka ya kuanzisha Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi ya Mahakama Kuu. Kwa mujibu wa muswada huo uliowasilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju, adhabu kwa watakaokutwa na hatia zimeongezwa, huku mahakama hiyo ikiwekewa mazingira wezeshi ili iendeshe kesi hizo kwa haraka. Mazingira wezeshi Muswada huo wa sheria ambao kwa sasa utakuwa ukisubiri Rais ausaini ili iwe sheria kamili, umekusudia kuanzisha divisheni hiyo ya mahakama, ambayo itakuwa na majaji wake na watumishi wake wanaojitegemea- HABARI LEO

 4. RC Makonda awa mbogo

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amefuta kibali cha shughuli za ujenzi cha Kampuni ya Ukandarasi ya Inshinomya Co. Ltd baada ya kubainika kujenga barabara chini ya kiwango. Kwa uamuzi huo, kampuni hiyo sasa haiwezi tena kufanya kazi za ujenzi wa barabara katika halmashauri zote za Jiji la Dar es Salaam. Sambamba na hatua hiyo, Makonda amesitisha zabuni ya ujenzi wa barabara kwa kampuni nyingine tatu za Germinex Construction Ltd, Del Monte (T) Ltd na Skol Building Contraction hadi atakapoamua vinginevyo- Mtanzania

5. Simba yamsainisha wa kuikomoa Yanga

Rais wa Simba Evans Aveva, amesikia mashabiki wanvyobabaika mittani kutokana na kelele za Yanga akawaambia ‘Tulieni, mchecheto wa nini wakati sie ndio viongozi wenu?’ kwa kuanzia amewaambua mashabiki kwamba yule straika wa Burundi ambaye Yanga walisikia anakuja Simba wakaanza kubabaika baadaye dili likaingia figisu, sasa ni uhakika msimu ujao anavaa uzi wa Mnyama. Huyu jamaa anaitwa Laudit Mavugo ana njaa ya magoli kinoma, unaambiwa. Aveva amesema wameshamaliza kazi- Mwanaspoti

6. Mpango wa kuuzia chakula Wagonjwa Muhimbili wasitishwa.

Ule mpango ulitotangazwa wa kuuzia wagonjwa Muhimbili chakula kwa Sh. 6000 kwa siku wagonjwa wanaolazwa katika hospitali ya Muhimbili kwa muda. Mpango huo umesitishwa leo Mjini Dodoma na Waziri wa afya Ummy Mwalimu, huku akisema inabidi Serikali ijiridhishe na jinsi mpango huo utakavyoenda. Amesema kwamba mwananchi hakushirikishwa vyema hivyo ameagiza uongozi wa serikali hiyo kuanza kutoa elimu kwa wananchi ili waelewe umuhimu wa mpango huo- Mwananchi

 

.

 

 

 

 

 

Comments

error: Content is protected !!