tmoja2

HARRIET TUBMAN: KUTOKA MTUHUMIWA HADI SURA KWENYE FEDHA YA MAREKANI.

275
0
Share:
Share this
tmoja2

Aliyekuwa Mwanaharakati wa haki za binadamu nchini Marekani Harriet Tubman sura yake itawekwa kwenye noti ya Dola 20 ya Marekani.

Harriet Tubman alizaliwa Machi 1822 Maryland Marekani na alifariki Machi 10 1913 New York akiwa na umri wa miaka 91. Uamuzi wa kuweka sura yake kwenye noti ya dola 20 umetangazwa leo na Sekretari wa fedha wa Marekani Jacob Lew. Hatua hiyo itamafanya Harriet Tubman kuchukua nafasi ya Adrew Jackson ambaye sura yake ndio iko kwenye noti hiyo kwa sasa.

23Harriet Tabman (1822-1913)

Harriet Tubman alikuwa mwanaharakati wa haki za binadamu na mtu aliyepinga vikali utumwa nchini Marekani. Alishiriki katika kuwatorosha watumwa kutoka Marekani kwenda Canada ambapo aliweza kuwahifadhi ili kukwepa mateso waliyokuwa wakiyapata Marekani. Aliweza kuwasaidiwa watumwa takribani 700 kupitia njia iliyochini ya ardhi. Alikuwa akifahamika kwa cheo alichopewa kama Musa wa watu weusi kwani kazi yake alihakikisha wanakua huru.

Uamuzi wa kumuweka sura ya Harriet Tubman kwenye noti ya Dola 20 ($20) unamfanya kuwa Mwanamke wa kwanza Marekani kuwa na sura yake kwenye noti kwa miaka 100. Suala hili limepokelwa kwa furaha kubwa na Wamarekani walio wengi hususani Wanawake kwani wamekuwa wakiona kwamba mchango wao katika maendeleo ya Marekani hautiliwi maanani.

Gazeti la New York Times Machi 1913 liliandika habari hii kuhusu Harriet Tabman

w

Comments

error: Content is protected !!