tmoja2

Harusi iliyogharimu kiasi cha shilingi bilioni 161

179
0
Share:
Share this
tmoja2

Nchini India, kumetoa ndoa iliyofungwa na kugharimu kiasi kikubwa zaidi cha fedha. Harusi hiyo ambayo ni ya binti wa mwanasiasa iliyogharimu kiasi kikubwa cha fedha hadi kufikia hatua ya kuzua mtafaruku ili hali watu wengi sana nchini humo wako katika hali ya umasikini.

Harusi hiyo iliyofanyika kwa siku tano ilifadhiliwa na mwekezaji mashuhuri ambae pia alikua Waziri katika jimbo moja India, G Janardhana Reddy.

Mwanasiasa huyo aliandaa sherehe hiyo kwa heshima ya binti yake aliyekua bibi harusi bi, Brahmani na iligharimu dola za Kimarekani milioni 74 (TZS bilioni 161.4).

Kadi za mwaliko zilirembwa kwa dhahabu, huku wageni wakitumbuizwa na wasanii kutoka Bollywood.

Watu wengi wamelalamikia harusi hiyo kama kejeli kwa masikini na onyesho la utajiri. Na cha ajabu zaidi Ilifanyika wakati serikali ya India ilipotangaza kuondoa Noti za rupee ya 500 na 1000 kama hatua ya nchi hiyo kuchunguza mali iliyopatikana kwa njia isiyo halali.

Bwana Reddy ametetea heshima yake kwa bintiye akisema ilimbidi kuuza baadhi ya mali zake zilizoko, Bangalore na Singapore ili kugharamia harusi hiyo. Aidha amesema malipo yote yalifanyika miezi sita kabla ya siku ya harusi.

Licha ya kujitetea , raia wengi wamelalamikia kitendo hicho kwenye mitandao ya kijamii.

Aidha, Bwana Reddy aliwahi kufungwa jela miaka mitatu kwa makosa ya ufisadi. Aliachiwa huru kwa dhamana mwaka uliopita. Hekalu ambapo harusi hiyo iliandaliwa zilirembeshwa kwa dhahabu na michoro maalum iliyotungwa na waandaa filamu kutoka Bollywood.

Reddy ametetea hatua ya kutumia fedha hizo kuandaa harusi ya bintiye

The bride's wedding sari cost £2million, while her jewellery cost another £10million

Comments

error: Content is protected !!