tmoja2

Hivi ndiyo Cristiano Ronaldo hutumia fedha zake zote

423
0
Share:
Share this
tmoja2

Kwa sasa Cristiano Ronaldo ndiye mchezaji anaelipwa zaidi ya wachezaji wa michezo yoyote. Kwa mshahara wa Real Madrid na mikataba mingine alioingia na makapuni kutangaza bidhaa zao zimemfanya awe ni mwenye fedha nyingi sana za kutupa.

Fahamu ni jinsi gani anazipata na anavyozitumia fedha hizo.

Ronaldo alijipatia dola milioni 88 (£ milioni 61) ndani ya kipindi ya miezi 12 iliyopita, ambazo zimemfanya kuwa mchezaji anaelipwa zaidi kwa mwaka huu kutokana na uchunguzi uliofanywa na jarida la Forbes.

Zaidi ya 1/3 hizo ($ milioni 32/£ milioni 22) inatokana na mikataba anayolipwa na kampuni kama Tag Heuer na Nike kwa kutangaza bidhaa zao.

Kwa dili la Nike pekee anavuta mkwanja mrefu tu wa zaidi ya  $13 m (£9 m). Na vile vile ana mikataba na kampuni kama Herbalife, Castrol, Samsung, and KFC

Mkataba wake mkubwa zaidi ni ule aliongia na Real Madrid, ambao unamlipa dola milioni 50 (£ 35mil.) kama mshahara wa mwaka na ziada. Na kama ataondoka Real Madrid, timu itakayomnunua itabidi iilipe klabu hiyo $1b (£690.5 m) kumnunua kabisa.

Anatumia fedha zake kwenye nini? Moja ya vitu anavypenda zaidi ni Ronaldo ni magari, anaendesha gari yenye thamani ya $ 300,000 (£ 207,000) aina ya Lamborghini Aventador pamoja na Maserati (pichani).

-

Na ameripotiwa kumiliki Bentley, Porsche, na Mercedes, pamoja na mengine.

--

Kwa kawaida huwa mwangalifu sana na magari yake, ijapokuwa mnamo mwaka 2009 alipata ajali akiwa kwenye  Ferrari yenye thamani ya  $320,000 (£221,000) akiwa Manchester.

Ronaldo anaishi ndani ya nyumba (Villa) yenye thamani ya dola 7.1 million (£5 million) huko La Finca — kijiji cha pekee kilichojengwa na mkandarasi Joaquin Torres huko Madrid.

---Eneo hilo ni  pazuri kupindukia/ kupita kiasi

----

Na ukiongelea kuhusu vitu anavyomiliki, amereipotiwa kununua apartment yenye thamani ya $18.5 million (£13 million) mwaka 2015 mijini Manhattan kwenye majengo ya Trump

Na vile vile ameonekana akivaa saa yenye thamani ya  $160,000 ya  Jacob and Co. hiyo yote ikiwa ni faida ya kuwa na mkataba na Kampuni hiyo.

-----

Na kuna ripoti zinasema kwamba Ronaldo ametumia  £20,000 ($29,000) kwa ajili ya ‘waxwork’ ya kwake mwenyewe kwenye ukumbi wake.

------

Maisha ya Fame na Mali nyingi yamefanya maisha ya mapenzi kwa Ronaldo kukumbwa na vitimbi mbalimbali na vyombo vya habari kwa Ronaldo. Alikua katika mahusiano ya kimapenzi na Irina Shayk mwanamitindo mzuri na muigizaji wa Kirusi kwa muda wa miaka 5 na kuachana nae mwanzoni mwa mwaka 2015.

Ronaldo pia ni mtu anaependa mitindo, hujisikia vyema  akivaa suti za bei kali amaye yeye huamin anapendeza zaidi kuliko akivaa nguo nyingine yoyote. Ronaldo ameshawahi kuwa mwanamitindo wa Armani, na vile vile ana bidhaa zake za nguo za kiume za ndani zilizobuniwa na Richard Chai ambazo zinatarajia kutoka hivi karibuni.

Licha ya hayo yoteUzuri wake haujawahi kukubalika kwa mashabiki wa timu pinzani kwake. Japo hilo halimsumbui, na alisema kwamba ‘nadhani sababu kubwa ni kwamba mie ni tajiri na pia nina muonekano mzuri na vile vile ni mchezaji mzuri ndio sababu kubwa ya watu hunionea wivu, sidhani kama kuna maelezo mengine zaidi ya hayo kwakweli’

Pia wakati mwingine huchangia katika jamii, mfano alipotoa mchango wa $165,000 (£114,000) kwenye ‘Portuguese cancer centre’ na  $83,000 (£57,000) kumsadia mtoto mwenye miaka 10 ili afanyiwe oparesheni ya Ubongo.

Comments

error: Content is protected !!