tmoja2

Huddah aeleza sababu ya kukataa kuja kwenye ‘party’ ya Diamond dakika za mwisho

207
0
Share:
Share this
tmoja2

Mrembo kutoka nchini Kenya, Huddah Monroe ameeleza sababu za kuingia mitini katika dakika za mwisho za show ya Wasafi Beach Party iliyofanyika siku ya mkesha wa Krismasi Jangwani Sea Breeze Dar es Salaam pamoja na iliyofanyika Iringa kwenye uwanja wa Samora.

Mrembo huo aliandika kupitia mtandao wa Snapchat kuwa anawapenda sana mashabiki zake kutoka nchini Tanzania na anawaomba msamaha kwa kushindwa kutokea kwatika tamasha hilo kwani yelishawekwa matangazo na yeye mwenyewe akakakiri angekuja na kuwataka mashabiki zake watokee kwa wingi.

Huddah aliandika “The last event is coz Diamond and I didnt agree on some issues, so i cancelled last minute. That’s the main reason.” akimaanisha kuwa hakuweza kuja kama alivyoahidi sababu yeye na Diamond hawakuwa wameafikiana kwenye baadhi ya mambo.

Mbali na Huddah, warembo wengi ambao wao walikuwepo ni pamoja na Vera Sidika kutoka Kenya na Anita Fabiola wa Uganda.

 

Comments

error: Content is protected !!