tmoja2

Instagram: Ujumbe wa Aunty Ezekiel kwa wanaosema anajipendekeza kwa Zari wa Diamond

11499
0
Share:
Share this
tmoja2

Baada ya picha kuenea mitandaoni mwisho wa wiki hii, ambapo Diamond Platnumz alipeleka familia yake Zanzibar kwenye kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa mama mtoto wake Zari Hassan huku akiwa na Dansa wake Mosee Iyobo ambaye naye aliongozana na mama mtoto wake Aunty Ezekiel.

Aunty Ezekiel ameonekana huko Zanzibar akiwa amepiga picha nyingi na familia hiyo na hivyo kuzua maneno katika mtandao wa Instagram huku watu wakisema anajipendekeza sana kwa mwanamke huyo wa Diamond ilahali yeye alikua na mahusiano mazuri na Wema Sepetu ambaye alikuwa ni mpenzi wa zamani wa Diamond.

Aunty ameamua kuwajibu haya wale wote wanaosema kuenda Zanzibar ni kujipendekeza kwa Familia ya Diamond na mama mtoto wake Zari.

#auntyezekiel – Naitwa Aunty Ezekiel Grayson jujuman Ukipenda …Mama Cookie Mnyakyusa hasilia …Sasa bac Nataka niwaambie kitu kimoja mana kujibu mmoja mmoja Muda huo sina ni hv Nafanya ntakalo sifanyi Mtakayo mana nina uhakika nyie mnaokaa kubishana na mm vibanda vya mbavu za zaMmbwa zinawashinda so muda mnaokaa mkafatilia yangu mngeenda tafuta lakufanya ….Oooh njaa Yes I say tena Yes mana mnataka nibadili Red kuwa Yellow kwani yule c ni boss wa mkata viuno wang au!!!Sasa kama ni boss ulitaka nibishe niseme mm ndio Boss bac nifungue band yetu acheze!!!Mnawazimu nn na Namuheshimu kama Mshkaji rafiki boss wa bwanaangu na siwezi acha kushirikiana na Familia yake eti kisa Ushuzi mtasema nn…Sitaki kutaja majina ya watu ila kilichopo ndio ukweli asilia Mama Tee ndio mwanamke na Mama watoto wa Nasibu no way hata tulambe rami kubadili ni ngumu Ila mwenyewe akibadili bac na Sisi tutabadili ila kwa sasa ni Mama tee Shukrani gud Day#msaliti kulingana na wakati eti umemuacha mumeo jela mlitaka nikagongane nae jela Au nikae miaka 20 akitoka nina miaka 50 nazaa lini nalea lini nakufa lini Wapuuzi nn msinichefue mie msitake niongee yasiyowahusu…Mnanitoa Povu kama mmenilaza kwenye sabuni ya Unga

aunty-eze

Comments

error: Content is protected !!