tmoja2

Kauli ya mama yake Diamond kuhusu hali ya kifedha

973
0
Share:
Share this
tmoja2

Licha ya mwanamuziki NasibAbdul maarufu Diamond Platnumz kuelezwa kuwa ana utajiri mkubwa, mama yake mzazi Sanura Kassim maarufu Sandra imedaiwa kuwa anaishi maisha magumu kiasi cha kupaki gari lake kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kukosa mafuta.

Kama lilivyoandika gazeti la Kiu, inaelezwa kuwa mama ya Diamond sasa hayuko vizuri kama alivyokuwa awali kwa baadhi ya huduma zimesitishwa kutoka kwa mwanae kutokana na hali ya kifedha kuwa mbaya. Miongoni mwa huduma zilizositishwa ni pamoja na, fedha kwa ajili ya kusuka nywele mara kwa mara, fedha za manunuzi ya vitu, vinywaji vya bei ghali, na kupungua kwa fedha za matumizi mengine.

Imeelezwa kuwa, chanzo cha kusitishwa kwa huduma hizo ni baada ya kupungua kwa fedha anazoingiza Diamond baada ya hali mitaani kuwa ngumu. Kutokana na hali hiyo mama Diamond akapaki gari yake aina ya passo kwani sasa hana misele mingi ya kumuingizia tena fedha.

Gazeti hilo liliendelea kueleza kuwa hata marafiki waliokuwa karibu na mama huyo wameanza kumkimbia baada ya hali kuwa ngumu huku ndugu wakichekelea kwa madai kuwa wakati mama huyo mambo safi alikuwa akiwapuuza na kuwaona hawana maana.

Aidha, mama Diamond alipoulizwa kuhusu taarifa hizi zilizozagaa mitaani alikanusha na kusema kuwa bado mwanae huyo anaendelea kumhudumia kama mwanzo na mambo ni mazuri hivyo habari kuwa wamefilisika ni umbea mtupu.

Comments

error: Content is protected !!