tmoja2

Kauli ya Rais Mstaafu Jakaya Kikwete kwa wanaotumia picha zake mitandaoni na kupotosha aliyoyasema

496
0
Share:
Share this
tmoja2

Watu mbalimbali katika mitandao ya kijamii wamekuwa wakitumia picha za watu maarufu ili kufikisha ujumbe fulani wakati mwingine ujumbe huo ukiwa ni mzuri na wakati mwingine huwa ni mbaya. Yote haya hufanywa ili mtu kuweza kufanikisha jambo analolitaka yeye.

Usiku wa kuamkia leo, kupitia akaunti yake ya Twitter, Rais Mstaafu wa Tanzania,Dkt. Jakaya Kikwete aliandika masikitiko yake juu ya namna watu wanavyotumia picha zake na kupotosha yale aliyoyasema ili kufanukisha matwaka yao ya kisiasa.

Aidha, Rais Kikwete aliwataka watu hao kumuacha kwani ameshamaliza muda wake wa uongozi hivyo ni wakati wake sasa kupumzika. Rais Kikwete pia alikanusha tuhuma za kuwa  anatofauti na Rais wa sasa Dkt John Pombe Magufuli na kusema kuwa anamuunga mkono Rais Magufuli pamoja na serikali yake.

Comments

error: Content is protected !!