tmoja2

Kizimbani kwa tuhuma ya kumuita Rais Magufuli ‘Kilaza’ kwenye kundi la WhatsApp.

2697
0
Share:
Share this
tmoja2

Mkazi mmoja wa jijini Dar es Salaam amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akituhumiwa kumuita Rais John Pombe Magufuli kuwa ni ‘Kilaza’ ujumbe alioutuma kwenye kundi la WhatsApp.

Elizabeth Asenga (40), amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na shtaka hilo ambapo wakati akisoma Shtaka hilo Wakili wa Serikali, Leonard Chalu mbele ya Hurum Shahidi alidai kuwa mtuhumiwa huyo alifanya kosa la matumizi mabaya ya Mtandao.

Aidha, wakili huyo alisema kuwa, Elizabeth alitenda kosa hilo kwa kuandika ujumbe huu;
“Good Morn humu , Nakuja Rais kilaza kama huyo wetu, angalia anampa Lissu umashahuli fala lile, Picha yake ukiweka Ofisini nuksi tupu ukiamka asubuhi ukikutana na picha yake kwanza siku inakuwa inamkosi mwanza mwisho.”

Baada ya kusomewa shtaka hilo, mtuhumiwa alikana shtaka hilo na kuachiwa kwa dhamana. Aidha upande wa Jamhuri ulisema kuwa upelelezi bado haujakamilika na shauri hilo litatajwa tena Septemba 22.

Comments

error: Content is protected !!