Mahusiano: Harmonize azungumzia kuachana na Wolper

3387
0
Share:
Share this
CMTL Group

Wiki iliyopita dalili za kuwepo vigisu vigisu katika penzi wa Jackline Wolper kutoka tasnia ya filamu na Harmonize kutoka katika tasnia ya muziki nchini Tanzania zilizanza kuonekana.

Wolper ndiye aliyekuwa wa kwanza kuonyesha dalili kuwa wawili hao wameachana baada ya kuweka picha ya Harmonize na kuandika¬† “Nina akili timamu me siyo mtoto mdogo, endelea na maisha yako it over waambie rasmi usifiche @harmonize_tz i hate love.”¬†Lakini Wolper hakuishia hapo bali alienda mbali na kufuta picha zote za Harmonize pamoja na zile za watu wengine kutoka WCB.

3

Muda wote huo Harmonize hakuwa amezungumza au kufanya chochote lakini leo amefunguka na kusema kuwa yote yanayofanyika anayaona mageni kwake kwani hajui chochote kinachoendelea.

Harmonize alipoulizwa kama ameachana na Wolper alisema yeye hajui chochote na kuwa labda akihojiwa mhusika mwenyewe (Wolper) anaweza akatoa majibu ya uhakika zaidi.

Lakini Harmonize alikiri na kusema kuwa ameona mpenzi wake huyo amefuta picha zake zote kwenye ukurasa wake wa Insagram lakini hajui kwanini amefikia hatua hiyo.

Harmonize na Wolper walianza uhusiano wao mwaka jana huku wakiwa wapenzi waliogonga vichwa vya habari mara kwa mara kutokana na sababu mbalimbali ambapo baadhi ya watu walidai kuwa wanatafuta kiki, wengine wakisema hawaendani.

 

Comments

error: Content is protected !!