Mahusiano: Wolper na Harmonize wameachana? Soma Wolper alichoandika Instagram

2158
0
Share:
Share this
CMTL Group

Walipoanza uhusiano wao wa kimapenzi, wengi walisema kuwa wanatafuta kiki na kwamba wanataka watu wawazungumzie sababu kuna filamu au wimbo mpya unakuja. Lakini baada ya muda kwenda na kuona mapenzi ya wawili hao yakiendelea kushamiri, watu waliamini ni kweli wanauhusiano wa kimapenzi.

Hapa namzungumzia malkia wa filamu Tanzania, Jackline Wolper na mwanamuziki kutoka WCB, Harmonize. Kadiri siku zilivyosonga wawili hawa walikuwa wakijiachia wazi wazi na kuonyesha namna walivyozama penzini.

Lakini huenda hali si shwari baina ya wawili hao kufuatia ‘post’ Wolper aliyoiweka leo kwenye ukurasa wake wa Instagram. Wolper aliweka picha ya Harmonize na kisha akaandika “Nina akili timamu me siyo mtoto mdogo, endelea na maisha yako it over waambie rasmi usifiche @harmonize_tz i hate love.”

3

Post hiyo haikuchukua muda kwenye ukurasa wake aliiondoa huku maswali yakibaki kuwa, Je! Ni kweli wameachana au wanatafuta kiki?

 

Comments

error: Content is protected !!