tmoja2

Majina ya Taasisi za Serikali zinazoongoza kwa madeni NHC.

2077
0
Share:
Share this
tmoja2

Serikali imetajwa kuwa kinara wa kukwepa kodi ya pango katika Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

NHC imetoa mwezi mmoja kwa makapuni yapatayo 29 ya taasisi mbalimbali za Serikali yaliyokwepa kulipa kodi, kulipa madeni yake kwa  Shirika hilo la nyumba la Taifa.

Miongoni mwa taasisi hizo zinazoongoza kudaiwa na NHC madeni  ambayo yamefikia zaidi ya Sh bilioni 9 ni:-

  1. Ofisi ya Rais inadaiwa zaidi ya Sh milioni 10.
  2. Wizara ya Uchukuzi inadaiwa zaidi ya Sh bilioni 2.
  3. Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi  yenye deni la Sh bilioni 2,
  4. Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo inayodaiwa zaidi ya Sh bilioni moja,
  5. Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inadaiwa zaidi ya Sh bilioni moja,
  6. Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, inadaiwa Sh milioni 613,
  7. Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora inadaiwa Sh milioni 360.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemiah Mchechu, alisema pamoja na deni hilo, zipo pia taasisi binafsi ikiwamo ile ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe.

Alisema Mbowe ambaye anaendesha Mbowe Hotel Ltd, maarufu Club Bilicanas iliyoko maeneo ya Posta, Dar es Salaam, anadaiwa zaidi ya Sh bilioni 1.1.

 

Comments

error: Content is protected !!