tmoja2

Makamu wa Rais, Samia Suluhu atembelea kiwanda cha A to Z Arusha

224
0
Share:
Share this
tmoja2

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema serikali itaendelea kuviimarisha vyuo vya ufundi stadi nchini –VETA- ili viweze kutoa wahitimu bora ambao watakidhi katika soko la ajira hasa kwenye viwanda vilivyopo na vitajengwa nchini.

img-20161125-wa0043

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo leo wakati anazungumza na uongozi wa kiwanda cha A to Z kilichopo mkoani Arusha katika ziara yake ambayo imeingia siku ya Pili ya kutembelea viwanda mbalimbali mkoani humo ili kujua changamoto zinazokabili viwanda hivyo na serikali kuzitafutia ufumbuzi.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema serikali imetenga fedha za kutosha zitakazotumika kuviimarisha vyuo vya Veta ili viweze kutoa mafunzo bora yatakayosidia vijana kufanya kazi zao kwa ufanisi wa hali ya juu pindi watakapoajiriwa au kujiajiri wenyewe.

img-20161125-wa0041

Kuhusu maslahi kwa wafanyakazi wa Kiwanda cha  A to Z,Makamu wa Rais  Samia Suluhu Hassan ameutaka uongozi wa kiwanda hicho kulinda na kutetea haki za wafanyakazi kwa kutoa maslahi mazuri ambayo yatawezesha wafanyakazi hao kufanya kazi kwa bidii.

Makamu wa Rais pia amesisitiza usawa katika ulipaji wa mishahara kwa wafanyakazi wa ndani na wa nje ya nchi walioajiriwa kwenye kiwanda hicho ili kuondoa tofauti za mishahara hali ambayo ijenga motisha kwa wafanyakazi.

img-20161125-wa0044

Kiwanda cha A to Z kilichopo eneo la Kisongo mkoani Arusha kimeajiri zaidi ya wafanyakazi 7500 ambapo asilimia 80 ya wafanyakazi wote ni wanawake.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewahimiza wawekezaji kote nchi walipe kodi za serikali mapema kodi ambazo zitatumika   kuimarisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

img-20161125-wa0047

Amewahakikishia wawekezaji kuwa Tanzania itaendelea kujenga na kuimarisha mazingira bora kwa wawekezaji ili kuhakikisha wawekezaji wanafanyakazi zao vizuri kwa ajili ya manufaa ya taifa na ya wawekezaji.

Imetolewa na

Ofisi ya Makamu wa Rais

Arusha

25-Nov-2016

Comments

error: Content is protected !!