Mapinduzi Cup: Azam yafanya kufuru Zanzibar, yaichakaza Yanga magoli 4-0

602
0
Share:
Share this
CMTL Group

Mchezo wa Kombe la Mapinduzi kati ya Yanga na Azam umemalizika muda huu katika uwanja wa Amani Zanzibar na Yanga kukubali kipigo cha mbwa mwizi.

Mchezo huo uliozikutanisha timu mbili za Tanzania Bara umemalizika kwa Yanga kufungwa magoli manne kwa sifuri na Azam. Mchezo huu ni wa kwanza kwa Yanga kupoteza katika michuano hii.

Magoli ya Azam yamefungwa na John Bocco aliyefunga goli la kwanza wakati goli la pili lilitiwa kimyani na Yahya Mohammed.

Magoli mengine yamefungwa na Joseph Mahundi aliyefunga goli la tatu na goli la nne kufungwa na Enock Agyei.

Comments

error: Content is protected !!