Mapinduzi Cup: Matokeo ya mchezo kati ya Yanga na Simba

858
0
Share:
Share this
CMTL Group

Klabu ya Simba ya Dar es Salaam imekata tiketi ya kushiriki fainali za kombe la Mapinduzi baada ya kuiadhibu Yanga kwa mikwaju ya penati 4-2 kufuatia timu hizo kutoka suluhu dakika 90 za mchezo.

Mchezo huu uliopigwa katika uwanja wa Amani Zanzibar ulivutia hisia za watu wengi kutokana na timu hizi kuwa na upinzani wa asili. Baada ya mchezo wa leo timu hizi zinakuwa zimekutana mara 6 huku Simba ikishinda mara 4 na Yanga mara 1 na kwenda sare mara 1 katika michuano hii.

Simba watakutana na Azam katika mchezo wa fainali ya Kombe la Mapinduzi inayotarajiwa kuchezwa Januari 13, 2017 katika uwanja wa Amani Zanzibar.

Azam wamefika hatua hiyo baada ya kwaondosha Taifa Jang’ombe kwa goli moja lililofungwa dakika ya 33 ya mchezo na Frank Domayo.

Comments

error: Content is protected !!