tmoja2

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema arejeshwa rumande

317
0
Share:
Share this
tmoja2

Mbunge wa Arusha Mjini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Godbless Lema leo amerejeshwa rumande baada ya kuletwa mahakamani kusikiliza uamuzi wa mahakama juu ya pingamizi lililowekwa na upande wa Jamhuri.

Lema amerejeshwa rumande hadi Disemba 16 mwaka huu ambapo Jaji anayesikiliza kesi hiyo atatoa uamuzi juu ya pingamizi hilo la jamhuri.

Uamuzi huo ulitarajiwa kutolewa leo mchana na Jaji Modesta Opiyo baada ya jana kupokea hoja za pingamizi la maombi hayo zilizotolewa na mawakili waandamizi wa Jamhuri katika shauri hilo, Paul Kadushi na Matenus Marandu pamoja na maombi ya mawakili wa Lema.

 

Comments

error: Content is protected !!