Mbunge wa CHADEMA ahukumiwa kifungo cha miezi 6 jela

627
0
Share:
Share this
CMTL Group

Mbunge wa Jimbo la Kilombero kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Peter Ambrose Lijualikali amehukumiwa kwenda jela kwa kipindi cha miezi sita baada ya kupatikana na hatia ya kufanya vurugu kipindi cha uchaguzi.

Mbunge huyo alifanya kosa hilo kipindi cha uchaguzi wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero mwezi Machi 2016 ambapo upinzani walilalamikia uchaguzi huo kuwa ulijawa vurugu na vitisho vya polisi.

Polisi walimkamata Mbunge huyo baada ya kudaiwa kuwa alitaka kuingia katika chumba cha kupigia kura wakati yeye hakuwa na haki ya kupigakura.

Ilidaiwa kuwa mbunge huyo alitakiwa kufika eneo hilo majira ya saa saba mchana ambapo alialikwa katika sherehe za ugawaji wa mali kati ya Halmashauri ya Mji wa Ifakara iliyozaliwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero lakini yeye alifika saa tatu asubuhi.

Comments

error: Content is protected !!