tmoja2

Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu alazwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Muhimbili

176
0
Share:
Share this
tmoja2

Mbunge wa Ilala, Azzan Mussa Zungu amelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)  baada ya kuzidiwa ghafka akiwa nyumbani kwake juzi.

Akizungumza na waandishi wa habari jana alisema kuwa anaendelea vizuri sasa baada ya kuzidiwa ghafla akiwa nyumbani kwake na kukimbizwa Hospitali ya Amana na baadae kupewa rufani ya kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili na kisha kuhamishiwa katika taasisi ya magonjwa ya moyo.

whatsapp-image-2016-12-02-at-9-43-34-am

Akielezea namna alivyopata na tatizo ghafla alisema kuwa akiwa nyumbani kwake majira ya saa nane mchana mapigo yake ya moyo yalipanda ghafla ndipo akapelekwa Amana.

Madaktari kwa sasa wanamfanyia uchunguzi wa tatizo la moyo na ndani ya siku tatu huenda akaruhusiwa kutoka.

Zungu aliupongeza uongozi na wafanyakazi wa taasisi hiyo kwa mapokezi na huduma nzuri wanazompatia huku akiwasihi kuwafanyia wananchi wote hivyo. Wakati huo huo Zungu ameipongeza serikali kwa ujenzi wa taasisi hiyo kwani zamani viongozi wengi walikuwa wakipelekwa nje ya nchi lakini sasa ni tofauti.

Comments

error: Content is protected !!