tmoja2

Mpango wa SUMATRA baada ya daladala zinazotoa huduma kati ya Mbezi na Hospitali ya Taifa Muhimbili kusitisha huduma zake

1773
0
Share:
Share this
tmoja2

Baada ya daladala zinazotoa huduma kati ya Mbezi na Hospitali ya Taifa Muhimbili kusitisha huduma kutokana na vibali vyao kwisha muda wake, abiria na wagonjwa wanaotumia njia hiyo wameiomba Mamlaka ya Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA), kuziacha gari hizo ziendelee kutoa huduma.

Abiria na wagonjwa hao walisema kuwa tangu magari hayo yaliposimamishwa siku sita zilizopita wanakumbana na changamoto ya usafiri kuwafikisha hospitalini hapo kwa ajili ya kupata huduma ya matibabu.

Mwenyekiti wa Chama cha Kutetea Abiria (CHAKUA), Hassan Mchanjama alisema ipo haja magari hayo kuongezewa muda hadi utakapopatikana ufumbuzi mwingine. Alisema kuondolewa kwa magari hayo kumewaongezea adha ikiwemo matumizi makubwa ya nauli ambayo wakati mwingine hayendani na kipato cha abiri na wagonjwa hao.

Alisema kutokana na mazingira hayo wapo baadhi ya abiria baada ya kushuka Fire inawalazimu kutembea kwa miguu ili kubana matumizi kwa ajili ya kubaki na fedha ya huduma hospitalini.

Akijibu malalamiko hayo, Meneja Mawasiliano wa Sumatra, David Mziray, alisema wanazo taarifa hizo na kwamba hivi sasa wanajipanga kuangalia uwezekano wa kuwapatia huduma hiyo haraka hadi hapo UDART watakapoanza kuelekeza gari zao huko.

Alisema wakati wakiendelea kutafuta suluhu ya tatizo hilo, itawabidi wananchi hao kutumia gari za kampuni ya UDART hadi Fire kisha kupanda daladala nyingine zinazotokea Temeke na Buguruni ili kufika hospitalini hapo.

 – HabariLeo

Comments

error: Content is protected !!