Mwanaume azikwa na fedha zake ili akamlipe Mungu kwa dhambi alizotenda duniani

559
0
Share:
Share this
CMTL Group

Mwanamume mmoja nchini Uganda amezikwa  na dola za kimarekani  5,700, ambazo alitaka kumlimpa Mungu ili ampe msamaha kwa dhambi zake alizofanya hapa duniani na kumuokoa kutoka kwa moto wa ahera.

Charles Obong, mfanyakazi wa zamani wa serikali (2006-2016) ambaye aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 52, aliomba hilo kwenye wosia wake, kwa mujibu wa familia yake.

Licha hayo kutekelezwa, kaburi lake lilifukuliwa na pesa hizo kuondolewa kutoka kwenye jeneza lake, baada ya wazee wa kazi kufahamu kilichotokea, kwa mujibu wa gazeti la the Daily Monitor.

Gazeti hilo lilimnukuu askofu mmoja wa kiangilikana Joel Agel, akisema hakuna pesa zinazoweza kununu uzima wa milele na Mungu hawezia kupokea pesa kama malipo.

Comments

error: Content is protected !!