tmoja2

Ndege ya Shirika la Ndege la Libya yatekwa ikiwa angani na watu 118

180
0
Share:
Share this
tmoja2

Ndege ya Shirika la Ndege la Afriqiyah ambayo hufanya safari zake ndani ya nchi ya Libya imetekwa na watu wawili wanaodai kuwa wanamabomu na hivyo watailipua ndege hiyo.

Ndege huyo Airbus A320 mali ya shirika la umma imetekwa ikiwa na watu 118 na ilikuwa ikitokea katika mji wa Sabha kwenda Tripoli na kubadilishwa njia huku ikitakiwa kutua Malta ambapo inaaminika kuwa uwanja huo wa ndege unashikiliwa na watu wao.

 

Safari zote za ndege kutoka na kuingia katika uwanja huo zimezuiwa huku nyingine zikielekezwa kutua sehemu nyingine.

Waziri Mkuu wa Malta aliandika kupitia ukurasa wake wa Twitter na kuutahadharisha umma kuhusu ndege hiyo iliyotekwa na kusema kuwa vyombo vya ulinzi vinafanyia kazi hali hiyo ya dharura.

Malta inapatikana umbali wa kilomita 30 Kaskazini mwa Mji wa Tripoli na karibu zaidi na Tunisia na ilishwahi kutumika tena kutua ndege iliyotekwa. Mwaka 1985 ndege Misri ilikuwa ikitokea Athens, Ugiriki kwenda Cairo nchini Misri na kulazimishwa kutua Malta ambapo kwa saa 24 ambazo ndege hiyo ilikuwa ikishikiliwa mateka 60 waliuawa.

 

Comments

error: Content is protected !!