tmoja2

Nyumba 10 zenye thamani zaidi duniani na wamiliki wake.

1171
0
Share:
Share this
tmoja2

10. 7 Upper Phillimore Gardens

Mahali ilipo: London

Thamani: $128 milioni

Ina vumba 10, Swimming pool iliyo chini, sauna, gym, ukumbi wa sinema, chumba cha kujifungia endapo wezi wataingia ili wasikudhuru.  na imepambwa kwa mabo, dhababu na kazi za sanaa mbali mbali.

Mmiliki: Kwa jina ni Olena Pinchuk ambaye ni mtoto wa Rais wa pili wa Ukraine Leonid Kuchma. Binafsi ni mwanzilishi wa wakfu ya ANTIAIDS na vilevile ni rafiki mkubwa wa Elton John.7-Upper-Phillimore-Gardens-London

9. Kensington Palace Gardens

Mahali ilipo: London

Thamani: $ 140 milioni

Ipo London Billionaires Row, na hivi karibuni itaingezewa uwanja wa kucheza tenesi chini ya nyumba hiyo, sehemu ya matibabu kama Dispensari na sehemu ya Makumbusho.

Mmiliki: kwa jina ni Roman Abramovich, ambaye ni bilionea huko Urusi na ni mmiliki wa kampuni ya uwekezaji binafsi ya Millhouse LLC. Na anajulikana zaidi kama mmiliki wa timu ya mpira ya Chelsea.

Kensington-palace

8. Seven The Pinnacle

Mahali ilipo: Big Sky, Montana

Thamani: $ 155 milioni

Ni nyumba kubwa sana katika klabu ya Yellowstone, klabu ya matajiri wanaocheza golf na kuruka kwenye mabarafu. sehemu zake za nyumba zote zina mfumo wa kutoa joto kwa sababu kuna baridi kali sana, swimming pool zaidi ya moja, gym, sehemu ya kuhifadhi mivinyi, na lift ya kupanda ili kuenda kuruka kwenye barafu kutokea juu.

Mmiliki: Edra na Tim Blixseth, ambao ni waanzilishi wa kampuni inayojihusisha na mali zisizohamishika kama nyumba au viwanja na pia mbao, Tim Blixseth ni mmojakati ya waanzilishi wa Klabu ya Yellowstone.

Seven-the-Pinnacle

7. Hearst Castle

Mahali ilipo: San Simeon, California

Thamani: $191 milioni

Nyumba ina vyumba 27, ilishawahi kutumika kwenye filamu ya The Godfather , Imeshawahi kukaribisha watu maarufu wengi sana ikiwemo, John na Jackie Kennedy, Clark Gable na Winston Churchill.

Mmiliki: Waangalizi wa William Randolph Hearst maana kwa sasa ni sehemu ya watalii na vile vile ni sehemu ya California Park System.

HEARST CASTLE

6. Ellison Estate

Mahali ilipo: Woodside, California

Thamani: $ 200 milioni

Ipo katika eneo lenye ukubwa wa hekari 23, kuna nyumba kumi, Ziwa la kutengenezwa na binadamu, kijumba cha kunywea chai, na nyumba ambayo imetengwa ajili ya kuogea, ‘bath house’.

Mmiliki: Larry Ellison ambaye ni mmoja wa waandilishi wa Oracle na mnamo mwaka 2013 alikua tajiri wa tatu duniani kwa mujibu wa Forbes.

o-LARRY-ELLISON-TAHOE-HOME-facebook

 

5. 18-19 Kensington Palace Gardens

Mahali ilipo: London

Thamani: $222 milioni

Nayo pia ni nyumba iliyopo Billionaires Row, Karibu kabisa na nyumba ya Prince William na Kate Middleton. Yenyewe ina vyumba vya kulala 12, mabafu yenye nakshi za Uturuki, Swimming pool ya ndani na sehemu ya kuegesha magari 20.

Mmiliki: Lakshmi Mittal, Kiongozi wa kampuni kubwa duniani ya kutengeza vyuma ya Arcelor Mittal, na kwa mujibu wa Forbes, yeye ni mmoja ya watu 100 matajiri India.

SECOND 18-Kensington-Palace-Gardens

4. Four Fairfield Pond

Mahali ilipo: Sagaponack, New York

Thamani: $248.5 milioni

Nyumba imejengwa kwenye eneo lenye ukubwa wa hekari 63, ina vyumba vya kulala 29, Vyoo 39, kiwanja cha kuchezea mpira wa kikapu, sehemu ya bowling na tenesi. swimming pool 3, na zaidi ina sehemu ya kulia chakula yenye ukubwa wa futi 91.

Mmiliki: Ira Rennert ambaye ni mmiliki wa Renco Group, na vile vile na mdau katika madini na vyuma.

Fairfield-Pond

3. Villa Leopolda

Mahali ilipo: Cote D’Azure. Ufaransa

Thamani: $750 milioni

imejengwa kwenye eneo lenye ukubwa wa hekari 50, kuna Green house kubwa, swimming pool yenye nyumba yake kwa pembeni, jiko la nje, sehemu ya kutua helikopta, na vile vile kuna nyumba ya kulala wageni kubwa kuliko nyumba za mamilionare wengi.

Mmiliki: Lily Safra yeye wenyewe ni mtu anayependa sana kusaidia watu wengine kwa kutoa michango panapostahili ( Philanthropist) na vile vile ni mjane wa William Safra.

villa_leopolda2_thumb

2. Antilia

Mahali ilipo: Mumbai India

Thamani: $ 1 bilioni

Unaweza ukasema sio nyumba kwa maana ina ghorofa 27, kwa chini kuna floor 6 za kupaki magari, kwa juu helikpta 3 zinatua, na inauhitaji wa watu 600 ili kuifanyia usafi na kuiweka sawa.

Mmiliki: inamilikiwa na tajiri mkubwa wa India Mukesh Ambani, mwenye thamani ya $ 23.6 bilioni (Forbes). Anaendesha viwanda vya Reliance.

ANTILIA

  1. Buckingham Palace

Mahali ilipo: London

Thamani: $1.55 bilioni

Ni nyumba anayoishi Malkia wa Uingereza na mnamo mwaka 2012 ilikadiriwa kuwa na thamani ya $1.5 bilioni, ina jumla ya vyumba 775, ambavyo kati yake 19 vinatumika kwa shughuli za kiserikali, 52 ni vyumba vya kulala, 188 ni vyumba vya wafanyakazi, ofisi 92 na vyoo 78.

Mmiliki: Serikali ya Uingereza – Malkia Elizabeth II, anayeongoza kuanzia mwaka 1952 mwezi Februari.buckingham-palace-tour-summer-opening-2015-ad00c5354eb7aff837932abb96167006

 

 

 

 

Comments

error: Content is protected !!