Orodha ya mabilionea 21 wa Afrika na thamani za utajiri wao wanaomiliki

4522
0
Share:
Share this
CMTL Group

Jarida a Forbes la nchini Marekani limetaja orodha ya mabilionea 21 kutoka barani Afrika ambapo ni nchi saba tu zilizopata nafasi ya kuingiza mabilionea kwenye orodha hiyo na Tanzania ikiwa mmoja wapo.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL), Mohammed Dewji (41) ametajwa kuwa miongoni mwa mabilionea 21 baada ya kuongoza vyema makampuni yaliyoanzishwa na baba yake miaka ya 1970.

Dewji amekuwa ndiye bilionea mwenye umri mdogo zaidi ambapo kwa wastani mabilionea wengine wanaumri wa miaka 63.

Dewji ameingia katika orodha hiyo na kushika nafasi ya 17 akiwa na utajiri wa dola bilioni 1.4 za kimarekani (zaidi ya TZS 2.8 trilioni) wakati bilionea kutoka Nigeria, Aliko Dangote ndiye anayeongoza orodha hiyo akiwa na utajiri wa dola za kimarekani bilioni 12.1.

Hapa chini ni orodha kamili ya mabilionea 21 wa Afrika na utajiria wao;

Namba Nchi Jina Utajiri
1. Nigeria Aliko Dangote Dola bilioni 12.1
2. Afrika Kusini Nicky Oppenheimer Dola bilioni 7
3. Nigeria Mike Adengua Dola bilioni 5.8
4. Afrika Kusini Johann Ruper & Family Dola bilioni 5.5
5. Afrika Kusini Christoffel Wiese Dola bilioni 5.5
6. Misri Nassef Sawiris Dola bilioni 5.3
7. Misri Naguib Sawiris Dola bilioni 3.7
8. Angola Isabela dos Santos Dola bilioni 3.2
9. Algeria Issad Rebrab % family Dola bilioni 3.1
10. Misri Mohamed Mansour Dola bilioni 2.7
11. Afrika Kusini Koos Beker  Dola bilioni 2
12. Morocco Othman Benjelloun Dola bilioni1.9
13. Misri Yaseen Mansour Dola bilioni 1.8
14. Nigeria Folorunsho Alakija Dola bilioni 1.6
15. Afrika Kusini Patrice Motsepe Dola bilioni 1.6
16. Morocco Aziz Akhannouch Dola bilioni 1.4
17. Tanzania Mohammed Dewji Dola bilioni 1.4
18. Misri Youssef Mansour Dola bilioni 1.1
19. Morocco Onsi Sawiris Dola bilioni 1.1
20. Morocco Anas Sefrioui Dola bilioni 1.1
21 Afrika Kusini Stephen Saad Dola bilioni 1.1

Comments

error: Content is protected !!