tmoja2

Picha 5: Ndege mpya ya Rwanda kubwa zaidi iliyozinduliwa mjini Kigali

7117
0
Share:
Share this
tmoja2

Ushindani wa safari za anga Afrika Mashariki na Kati unazidi kuwa mkubwa baada ya shirika la ndege la Rwanda, RwandAir, kuzindua ndege yake mpya aina ya Airbus A300-200.

Ndege hiyo kubwa ya Rwanda iliyonunuliwa nchini Ufaransa ina uwezo wa kubeba abiria 244 hivyo kuongeza ushindani katika safari za anga ndani na nje ya Rwanda.

Ndege hii imenunuliwa dola milioni 200 za Marekani na ilizinduliwa kwa mara ya kwanza kwenye uwanja wa kimataifa wa Kanombe, Kigali.

Ndege hiyo ina uwezo wa kubeba abiria 244

Shirika la ndege la Rwanda sasa litakuwa limejipanua wigo wa safari zake na kuanza kufanya safari zake kwenda barani Ulaya, Asia na Kusini mwa Afrika tofauti na ilivyokuwa awali. Safari ya kwanza ya ndege hii itakuwa Oktoba 8 mwaka huu ambapo ndege hiyo itakwenda nchini Dubai.

Picha zaidi.Ndege ya RwandairRwandairSafari ya kwanza ya ndege hiyo itakuwa kwenda DubaiRwandair

Comments

error: Content is protected !!