Picha 8: Muonekano wa sasa wa Jennifer na Patrick walioibuliwa na marehemu Steven Kanumba

5119
0
Share:
Share this
CMTL Group

Watu wengi watawakumbuka Jennifer na Patrick kwa jinsi walivyoweza kutikisa tansia ya filamu Tanzania kipindi cha nyuma walipoibuliwa na marehemu Steven Kanumba.

Watoto hawa wawili walicheza kwa ustadi mkubwa katika filamu za Uncle JJ na This is It zote za marehemu Kanumba.

Kwa sasa Hanifa Daud ‘Jennifer’ na Othman Njaidi ‘Patrick’ si watoto tena. Wawili hawa hawajaonekana sana kwenye filamu baada ya Steven Kanumba aliyewatoa kufariki.

Jennifer ambaye amehitimu kidato cha nne mwaka jana mara ya mwisho alionekana kwenye filamu ya Zena na Betina ya Salma Jabu a.k.a Nisha mwaka 2014. Kwa upande wake Patrick, yeye alisema kuwa hana shauku ya kuigiza tena kama ilivyokuwa awali.

Picha: Bongo5

Comments

error: Content is protected !!