tmoja2

Picha: Rais Magufuli na mkewe washiriki ibada ya Krismasi mkoani Singida

305
0
Share:
Share this
tmoja2

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Mkewe, Mama Janeth Magufuli, leo tarehe 25 Desemba, 2016 wameungana na waumini wa Jimbo Katoliki la Singida kusali Misa ya Krismasi iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Moyo Mtakatatifu wa Yesu Mjini Singida.

img_20161225_145626

Misa hiyo Takatifu ya Krismasi imeongozwa na Askofu wa Jimbo Katoliki la Singida Mhashamu Edward Mapunda.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa Misa Takatifu, Mhe. Rais Magufuli amewatakia heri ya Krismasi waumini wote wa Jimbo la Singida na Watanzania wote kwa ujumla na amewasihi kusherehekea kuzaliwa kwa Bwana Yesu kwa kuendeleza amani na upendo na kuacha vitendo vya kubaguana kwa misingi ya dini, kabila, itikadi na kanda zao.

img_20161225_145630

Dkt. Magufuli amewahimiza Watanzania wote kuongeza juhudi katika kuchapa kazi kama alivyofanya Bwana Yesu na pia amesema kwa kuwa maeneo mengi ya nchi yameonekana kukabiliwa na uhaba wa mvua, ni vema wakatumia vizuri mvua chache zinazoendelea kunyesha kuzalisha mazao yanayokomaa haraka ili kuepuka upungufu wa chakula.

img_20161225_145635

Kwa upande wa Mkoa wa Singida ambao ni maarufu kwa kilimo cha alizeti, Mhe. Rais Magufuli amewasisitiza kuchangamkia fursa ya ujenzi wa viwanda ambayo nchi inatoa kipaumbele kwa kuzalisha alizeti kwa wingi ili zitumike kuzalisha mafuta ya kupikia kwa wingi.

img_20161225_145639

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mke wake Mama Janeth Magufuli wakiwa katika Misa ya Krismasi katika Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida.
                                                                                    
Rais Magufuli na mkewe wakisilkiliza neno Hapa wakiwa katika sala.

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwasalimia waumini wa Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida mara baada ya kushiriki Misa ya Krismasi katika kanisa hilo mkoani Singida

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia waumini wa Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida mara baada ya kushiriki Misa ya Krismasi katika kanisa hilo mkoani Singida.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Baba Askofu wa Jimbo la Singida Askofu Edward Mapunda mara baada ya Ibada ya Krismasi katika Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Baba Askofu wa Jimbo la Singida Askofu Edward Mapunda mara baada ya Ibada ya Krismasi katika Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida.

Baba Askofu wa Jimbo la Singida Askofu Edward Mapunda akimuombea na kumbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya Ibada ya Krismasi katika Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli wakisalimiana na waumini wa Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida mara baada ya ibada ya Krismasi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli wakipunga mkono wakati wakitoka kwenye Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida. PICHA NA IKULU

 

Jaffar Haniu

Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Singida

25 Desemba, 2016

Comments

error: Content is protected !!