tmoja2

Picha: Roketi kubwa zaidi kuwahi kuundwa nchini China

393
0
Share:
Share this
tmoja2

Taifa la China Limerusha angani roketi kubwa zaidi kuwahi kuundwa katika taifa hilo, roketi iliyopewa jina Long March 5.

Roketi hiyo ilirushwa angani kutoka kituo cha shughuli za anga za juu cha Wenchang katika mkoa wa Hainan na Imebeba setilaiti ya kufanya majaribio ambayo imepewa jina Shijian-17.

Long March 5 imeifanya nchi ya China kuwa na uwezo wa kupeleka angani mitambo na mizigo mizito, kwa mfano mitambo ya kutumiwa kwa ajili ya mawasiliano na vifaa vya kuunda kituo cha anga za juu ambacho taifa hilo linapanga kujenga.

Shirika la anga za juu la Marekani (Nasa) pia linakaribia kufanya safari ya kwanza ya roketi kubwa ambayo wanasema ina uwezo wa kubeba tani 130 hadi sasa.

Nasa imesema itatumia roketi hiyo kutuma wana anga hadi sayari ya Mars. Safari ya kwanza ya roketi hiyo imepangiwa kufanyika 2018.

Rocket

Image result for Long March 5

– BBC

Comments

error: Content is protected !!