tmoja2

Picha: Waziri ardhi afungua Baraza la Ardhi na Nyumba la Mkoa wa Kigoma

252
0
Share:
Share this
tmoja2

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, WilliAm Lukuvi anaendelea na ziara ya siku tatu katika mkoa wa Kigoma ambapo amefungua rasmi Baraza la Ardhi na Nyumba la Mkoa wa Kigoma pamoja na kutatua migogoro ya ardhi ya wananchi wa Kigoma.

Wananchi hao wamempongeza Waziri Lukuvi kwa hatua anazozichukua katika kumaliza migogoro yao ya ardhi na kuwajengea Baraza la Ardhi na Nyumba ambalo ni jipya na lililo na viwango kushinda mengine yote hapa nchini.

1-4Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akifungua Baraza la Ardhi na Nyumba la Mkoani Kigoma, Kushoto ni Mbunge wa Kigoma Mjini  Zitto Kabwe na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Emanuel Maganga. 2-1 2-2 Jengo jipya la Baraza la Ardhi na Nyumba la Mkoani Kigoma. 3-1 3-3Samani mpya za Baraza la Ardhi na Nyumba la Mkoani Kigoma. 4 4 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,  William Lukuvi akiongea na wananchi wa Kigoma Mjini na kutatua migogoro yao ya ardhi. 5Wananchi wa Kigoma Mjini wakiwasilisha malalamiko yao ya migogoro ya ardhi kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ili yaweze kutatuliwa. 7-1 7-2Wananchi wa Kigoma mjini wakimsikiliza Waziri wa Ardhi.

 

Comments

error: Content is protected !!