tmoja2

Polisi wazuia mkutano wa CHADEMA Chalinze dakika chache kabla haujaanza.

214
0
Share:
Share this
Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limezua mkutano wa hadhara wa CHADEMA uliopangwa kufanyika katika Uwanja wa Miembe Saba mjini Chalinze.
Awali Jeshi la Polisi liliruhusu uwepo wa mkutano na kutuma nakala ya barua ya kukubali ombi la viongozi hao. Akizungumza mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Pwani alisema alishangazwa na hatua hiyo ya polisi kwa kuwa mkutano huo ulifuata taratibu zote na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Chalinze, aliruhusu kufanyika kuanzia saa 6.00 mchana hadi saa 12.00 jioni.
Alisema kuwa walishajiandaa tayari kwa mkutano huo huku wananchi waki wanaanza kufika ndipo walipoitwa Polisi na kuambia mkutano huo hauwezi kufanyika kwa maelezo kuwa intelijensia ya polisi imeonyesha kuwa viongozi wengi wa kitaifa wangehudhuria kwenye mktano hui na wao (polisi) hawajajipanga kutoa ulinzi kwa viongozi hao.
Kwa mujibu wa viongozi wa CHADEMA, Kiongozi pekee wa kitaifa ambaye angehudhuria mkutano huo ni Mjumbe wa Kamati Kuu mwenye makazi yake mkoani humo, Fredrick Sumaye.
Hapa chini ni nakala ya barua ya kuruhusiwa kufanya mkutano.
1 (1)

Comments

error: Content is protected !!