tmoja2

Sugu (Mb) adaiwa kuwatukana wabunge wa CCM Bungeni jana

153
0
Share:
Share this
tmoja2

Mbunge wa jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (CHADEMA) maarufu Sugu, jana alizua utata Bungeni baada ya kuonyesha alama kwa wabunge wa CCM ambayo ilutafsiriwa kuwa ni tusi kwa wabunge hao.

Wakati wabuge wa upinzani walipokuwa wakitoka nje ya ukumbi wa Bunge jana, inadaiwa kuwa mbunge huyo alionyesha alama ya kidole cha kati ambacho huelezwa kuwa ni tusi kwa wabunge wa CCM walibaki ukumbuni.

Sugu alifanya tukio hilo baada ya wabunge waliokuwamo ukumbini kuwazomea wabunge wa upinzani ambao wamekuwa wakitoka nje pindi Naibu Spika, Dkt Tulia Ackson anapoongoza Bunge kwa madai ya kutokuwa na imani naye.

Aidha, baada ya taarifa kufikishwa kwa Naibu Spika, alisema kuwa hawezi kutoa maamuzi kwa sababu hakushuhudia kitendo hicho. Lakini aliahidi kwenda kufuatilia mkanda wa video wa siku hiyo kuona kama ni kweli kitendo hicho kilifanyika na ndipo atakapoweza kutoa maamuzi.

Comments

error: Content is protected !!