tmoja2

Taarifa kutoka Ikulu: Rais Magufuli akutana na Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Thabo Mbeki

614
0
Share:
Share this
tmoja2

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 14 Novemba, 2016 amekutana na Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Mhe. Thabo Mbeki ambapo viongozi hao wawili wamezungumzia masuala mbalimbali kuhusu Umoja wa Afrika (AU).

Pamoja na kuzungumzia masuala yahusuyo Umoja wa Afrika, Rais Mstaafu Thabo Mbeki amempongeza Rais Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Rais Mstaafu Thabo Mbeki pia amempongeza Rais Magufuli kwa juhudi kubwa alizozifanya katika uongozi wa nchi kwa kipindi cha mwaka mmoja aliokuwa madarakani.

Kwa upande wake Rais Magufuli amemshukuru Rais Mstaafu Thabo Mbeki kwa kumtembelea na kufanya nae mazungumzo na pia amempongeza kwa kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Usomi na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

14 Novemba, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Thabo Mbeki mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Thabo Mbeki mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mwenyeji wake Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Thabo Mbeki kabla ya kuanza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mwenyeji wake Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Thabo Mbeki mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Thabo Mbeki mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

Comments

error: Content is protected !!