Timu zitakazoshiriki Kombe la Dunia zaongezwa na kufikia 48

399
0
Share:
Share this
CMTL Group

Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) leo limepitisha mapendekezo yaliyokuwa yakilenga kuongeza timu zitakazoshiriki Kombe la Dunia na kufikia timu 48.

Kufuatia kikao kilichofanyika leo, FIFA wamepitisha kuwa kuanzia mwaka 2026 timu zitakazoshiriki zitakuwa 48 ambapo kutakuwa na makundi 16 huku kila kundi likiwa na timu 3. Katika makundi hayo ni timu 2 tu kwa kila kundi zitakazoingia hatua ya mtoano. Kwa mantiki hiyo, hatua ya mtoano itakuwa na timu za mataifa 32.

Germany won the World Cup back in 2014 - the tournament will soon have 48 teams

Bara la Afrika na Asia pia yatanufaika na mpango huu sababu idadi ya timu zitakazokwenda kushiriki kombe la dunia zitaongezeka.

Mpango huo ambao ulipigiwa chapuo na Rais wa FIFA, Gianni Infantino umepitishwa kwatika kikao kilichofanyika mjini Zurich ikiwa ni baada ya kutolewa tuzo za FIFA.

How the World Cup will look from 2026 after FIFA agreed to increase the number of teams 

Hadi kufikia hatua ya kupitisha pendekezo hilo moja, kulikuwa na mapendekezo matano yaliyojadiliwa na wananchama 37 wa FIFA.

  • Kombe la Dunia lenye timu 48 na makundi 16 ya timu tatu kila kundi ambapo timu mbili bora zitasonga kwa hatua ya muondoano ya timu 32 (mechi 80 kwa jumla).
  • Kombe la Dunia la timu 48, mechi moja ya muondoano wa kufuzu ambapo mshindi atajiunga na timu 16 nyingine (mechi 80 kwa jumla – 16 za muondoano wa kufuzu na 64 za michuano kamili).
  • Kuwa na timu 40 na makundi 10 ya timu nne kila kundi ambapo mshindi, na timu sita pekee zinazomaliza nambari mbili kundini ndizo zinafuzu (mechi 76).
  • Kuwa na timu 40 na makundi manane ya timu tano kila kundi (mechi 88).
  • Kusalia na Kombe la Dunia lilivyo sasa ambapo kuwa timu 32 (mechi 64).

Comments

error: Content is protected !!