Ujumbe wa Diamond alioandika kwenye picha ya mwanae Tiffah wawakera watu

849
0
Share:
Share this
CMTL Group

Mwanamuzi anayetamba nchini Tanzania, Nasib Abdul maarufu Diamond Platnumz amezua gumzo kwenye mitandao ya kijamii kufuatia ujumbe (caption) aliyoiweka chini ya picha ya mwanae ‘Tiffah’ kwenye ukurasa wake wa instagram.

Diamond alipoweka picha ya mwanae aliandika mananeyo yanayo someka hivi:- “Buff day Girl! my little Pumpkin? My Miss World ? @princess_tiffah kua mama, nikupe Raha ya Dunia na ujifaidie Ustar wako….. ila dah ukikua chonde mama ukitunze wasikile sana #KIDOGO tu, Maana ntalificha wapi hili sura langu.”

Kikubwa kilichozua zogo ni kipande cha ujumbe huo chenye maneno ila dah ukikua chonde mama ukitunze wasikile sana #KIDOGO tu.” Baadhi ya watu wakihoji kwanini mtu mzima amuandike mtoto maneno kama hayo?

Watu wamekerwa na maneno yake wakisema kwanini mtoto mdogo kama huyo unaanza kumuwazi habari za ngono wakati hata mwaka mmoja hajafikisha.

Wapo waliomshauri wakimtaka amuombee mwanae akue vema badala ya kuandika mambo hayo kwenye miandao ya kijamii.

Diamond mwenyewe hajasema hasa alichokimaanisha kwa maneno hayo yaliyoonekana kuwakera mashabiki zake.

Comments

error: Content is protected !!