tmoja2

Utafiti: Unene huuwa wanaume mapema zaidi kuliko wanawake.

131
0
Share:
Share this
tmoja2

 

Utafiti wa kimataifa umegundua kuwa Unene umekua ni sababu kubwa vifo vingi vinavyotokea kabla ya wakati (umri mdogo) huku wanaume wakiwa katika uwezekano mara tatu wa kufariki zaidi ya wanawake.

Kwa kutumia data za utafiti uliofanywa kwa takriban watu milioni 4 kutoka mabara manne tofauti, Utafiti huo uliochapishwa katika jarida la Lancet unaashiria kwamba watu wanene wanakufa kwa kiasi cha miaka mitatu mapema tofauti na watu walio na unene wa kawaida.

Watu wenye unene wa kupindukia inaonekana hupoteza miaka kumi ya maisha yao ambayo wangeweza kuishi endapo wangepunguza kilo za mwili wao.

Wanasayansi wanasema kwamba kuwa na uzito mkubwa wa mwili kunaongeza hatari ya kuugua maradhi ya moyo na ya mapafu, kiharusi na saratani.

Na ikumbukwe kwamba utafiti huo mpya unatofautiana na matokeo ya utafiti wa awali yaliyoashiria kwamba kuwa mnene kuna manufaa ya kuishi zaidi.

Badala yake watafiti wanasema moja kati ya vifo 5 vinavyotokea kwa watu wenye umri mdogo nchini Marekani na moja kati ya vifo 7 vya aina hiyo hiyo Ulaya, vinatokana na kunenepa kupindukia.

 

Comments

error: Content is protected !!