Video: Alichosema Samatta baada ya rafiki yake Wilfred Ndindi kusajiliwa Leicester City

573
0
Share:
Share this
CMTL Group

Januari 5 mwaka huu klabu ya Leicester City ya nchini Uingereza ilikamilisha usajili wa mlizi wa kati raia wa Nigeria kutoka klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji, Wilfred Ndindi.

Ndindi mwenye umri wa miaka 20 alikamilisha usajili wake siku ya Alhamisi baada ya kupata kibali cha kufanyakazi nchini Uingereza. Amesajiliwa kwa TZS bilioni 40.3 ambapo alidondoka saini mkataba wa miaka mitano na nusu.

Image result for Samatta and Ndindi

Akizungumza na Idhaa ya Kiswahili ya BBC, mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta anayekipiga katika klabu ya KRC Genk amesema kuwa anafuraha kwamba Ndindi ambaye ni rafiki yake amepiga hatua kubwa katika suala la mpira japo atabaki mpweke kwani alikuwa amemzoea sana.

Samatta aliyasema hayo alipoulizwa maoni yake kuhusu Ndindi kusajiliwa Leicester City. Aidha alisema kuwa hiyo ni changamoto kwake kwani inamfanya na yeye afanyekazi kwa bidii aweze kufikia hatua hiyo na zaidi.

Ndindi tayari amefanya mazoezi na wachezaji wengine wa Leicester na huenda akacheza leo kwa mara ya kwanza katika mchezo wa kombe la FA dhidi ya Everton.

Ndindi aliisaidia klabu yake ya Genk kumaliza katika nafasi ya kwanza katika hatua ya makundi ya michuano na Europa na kuihakikishia timu hiyo nafasi katika hatua ya mtoano.

Comments

error: Content is protected !!