Video: Avaa dera la mkewe baada ya kupigiwa simu ya pesa ghafla

476
0
Share:
Share this
CMTL Group

Januari watu wengi huuona kuwa ni mwezi mgumu hasa kwa vile ndio watu wametoka kwenye sikukuu za mwisho wa mwaka na unapoanza tu mwezi huu basi majukumu kibao yanakuandamana. Wale wa kulipa kodi basi ndio mwezi huu, watoto wanafungua shule, baada ya likizo unatakiwa kurudi kazini na wengine ndio kipindi cha kuandaa mashamba.

Kwenye suala la uchumi watu hushikika ile mbaya kiasi kwamba wakipata michongo ya fedha basi wanahakikisha haipotei. Kituko hiki kimetokea uswahili ambapo jamaa amevaa dera la mkewe kwa furaha baada ya kupigiwa simu ya pesa.

Uswahilini ni sehemu ambayo inaongoza kwa vituko, ugomvi na maneno ya shombo. Wahenga walisema kuishi kwingi ndio kuona mengi, Haraka Haraka haina baraka hii misemo inamaanaisha ukiishi sehemu tofauti tofauti utaona vitu vingi na kujifunza pia. Haraka haraka haina baraka hii imebeba maana ya kwamba ukienda haraka unaweza kukosea au kusahau kitu muhimu.

Tazama kisa chote hapa chini.

Comments

error: Content is protected !!