Video: Diamond na Rayvanny walivyoimba ‘live’ wimbo wa Salome kwenye tuzo za CAF Nigeria jana

584
0
Share:
Share this
CMTL Group

Usiku wa kuamkia leo Shirikisho la Soka Afrika (CAF) lilitoa tuzo za mwaka kwa wachezaji, viongozi na vikundi mbalimbali vilivyofanya vizuri kwa mwaka 2016.

Kwa upande wa Tanzania hatukupata tuzo yoyote lakini hatukutoka mikono mitupu kwani mwanamuziki Diamond Platnumz na Rayvanny walitumbuiza katika hafla hiyo ya utoaji tuzo na kuzidi kupeperusha bendera ya taifa na kuitangaza sanaa ya Tanzania na lugha ya kiswahili.

Diamond alitumbuiza wimbo wa Salome aliomshirikisha Rayvanny ambao ni wimbo uliofanya vizuri sana kwa mwaka 2016. Hapa chini ni video ya wawili hao walipotumbuiza katika hafla hiyo iliyofanyia Abuja nchini Nigeria Januari 5.

Comments

error: Content is protected !!