Video: Goli la maajabu lililoshinda tuzo ya FIFA ya Goli Bora la mwaka 2016

754
0
Share:
Share this
CMTL Group

Mchezaji wa Malaysia, Mohd Faiz Subri alishinda tuzo ya Puskas ya FIFA kufuatia goli lake bora alilolifunga katika ligi kuu ya nchi hiyo Februari 2016.

Subri was given the Puskas Award for his spectacular free-kick against Pahang

Mohd alifunga goli hilo Februari 16, 2016 kwa mpira wa adhabu alioupiga na kuandikia timu yake ya Penang goli dhidi ya Pahang zote za ligi kuu ya Malaysia.

Goli hilo liliwashangaza wengi sababu mpira ulipigwa kana kwamba unatoka nje lakini ulipinda na kuzama nyavuni huku kipa akibaki kushuhudia nyavu zikitikisika bila kujua muujiza gani ulitokea.

Mohd alikabidhiwa tuzo hiyo na mchezaji nguli wa Brazil Ronaldo katika hafla iliyofanyika mjini Zurich Januari 9 mwaka huu.

Mohd Faiz Subri was given the award for his amazing swerving free-kick against Pahang 

Litazame hapa chini goli bora la FIFA mwaka 2016.

Comments

error: Content is protected !!