tmoja2

Video: Kisiwa kinachoelea ndani ya ziwa Victoria kikisogea hadi kwenye ufukweni.

4480
0
Share:
Share this
tmoja2

Kisiwa kinachoelea ndani ya Ziwa Victoria kikisogea hadi kwenye ufukwe wa Speke eneo la Munyonyo nchini Uganda. Baadhi wa wananchi wakajitokeza kushangaa maajabu hayo.

Kisiwa hicho kilijitoka katika nchi kavu mwaka 2015 na kimekua kikihama kwenda maeneo tofauti tofauti. Mkazi mmoja wa nchini Uganda ambaye alikuwa akifanya kazi za kilimo katika eneo hilo alisema alishangaa kuja asubuhi na kukuta eneo la shamba alilolima jana halipo.

Mamlaka nchini Uganda zimewaonya watu wanaoishi katika kisiwa hicho kuwa wanahatarisha maisha yao lakini wao wameeleza kuwa wapo salama kwa huwa hawakisikii kikisogea.

Baadhi yao wamekuwa na makazi ya kudumu katika kisiwa hicho lakini baadhi huja na mitumbwi na kuishi hapo ka siku kadhaa kisha kuondoka. Nyumba nyingi zilizopo katika kisiwa hicho ni za nyasi.

Man coming out of grass house

Kisiwa hicho kimepewe jiana la Mirembe likimaanisha ‘Amani Luganda’, na watu wamekua wakiendesha shughuli mbalimbali za kilimo.

A sign saying

Comments

error: Content is protected !!