Video: Mtoto wa miaka miwili amuokoa pacha wake baada ya kuangukiwa na kabati

601
0
Share:
Share this
CMTL Group

Matukio kadhaa ya watoto kufariki dunia kutokana na kuangukiwa na samani za ndani kama vile kabati, meza, makochi au runinga yamekuwa yakiripotiwa katika maeneo mbalimbali.

Chanzo cha vifo hivi mara nyingi hutokea pale mtoto au watoto wanapokuwa wanachezea samani hizo na mwishowe huwaangukia na kusababisha kupoteza uhai.

Hapa chini ni video iliyozua hisia za watu wengi ambapo anaonekana mtoto wa miaka miwili akisogeza kabati ili pacha mwenzake atoke baada ya kuangukiwa na kabati walipokuwa wakicheza.

Brock na Bowdy Shoff wanaokana wakipanda kwenye droo za kabati na ghafla kabati inaanguka. Bowdy anafanikiwa kutoka lakini pacha wake Brock anabaki chini sababu amebanwa na kabati na kwa bahati nzuri kichwa chake kinakuwepo sehemu yenye uwazi na si kugandamizwa kwenye sakafu.

Tukio hili limetokea nchini Marekani ambapo kwa sasa kuna kampeni ya ‘ Anchor it‘ ambayo inawataka wazazi kuhakikisha vitu kaba kabati, runinga na vitu vingine vyenye uwezo wa kuanguka vifungwe ukutani.

Comments

error: Content is protected !!