Video: Rais Dkt. Kikwete akicheza wimbo wa Matatizo wa Harmonize

681
0
Share:
Share this
CMTL Group

Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete atakumbukwa kwa mengi lakini moja wapo ni jinsi alivyojikita kuinua vipaji vya watu wengi kuanzia kwenye mpira, muziki na hata filamu wakati akiwa madarakani.

Mara kadhaa Rais Kikwete alikuwa akikutana na wasanii Ikulu, Dar es Salaam lakini pia wachezaji mbalimbali hasa pale wanapokuwa wamenyakua tuzo na kuiletea sifa Tanzania na kuitangaza sanaa ya Tanzania.

Siku ya Mwaka Mpya, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete alikutana na mwanamuziki Harmonize kutoka WCB ambapo pia katika video iliyoweka na Harmonize kwenye ukurasa wake wa Instagram, Rais Kikwete anaonekana alihudhuria tamasha ambalo Harmonize alitumbuiza katika Sikukuu ya Mwaka Mpya.

Video hiyo inamuonyesha Rais Kikwete na Mkewe, Salma Kikwete wakicheza wimbo wa Matatizo wa Harmonize katika usiku wa mwaka mpya.

Hapa chini ni video ya Harmonize alipokutana na Rais Kikwete.

Majaliwa yake Mungu kuuona mwaka tuseme Ameen ?

A video posted by Harmonize (@harmonize_tz) on

Comments

error: Content is protected !!