tmoja2

Video: Rais Mugabe ashindwa kuchota udongo na kuweka ndani ya shimo la mti

349
0
Share:
Share this
tmoja2

Kupitia mitandao ya kijamii, imesambaa video ya Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe akipanda mti katika sherehe ya siku ya kupanda miti nchini humo.

Kikubwa katika video hiyo si kuonyesha Rais Mugabe akipanda mti tu, ni jinsi alivyokuwa akijitahidi kuchota udongo kwa kutumia beleshi kuweka ndani ya shimo la mti bila mafanikio. Mkewe, Grace Mugabe aliyekuwa pambeni yake ndiye aliyemsaidia kuchota udongo na kuuweka ndani ya shimo.

Watu wengi walioweka video hiyo kwenye mitandao ya kijamii wamemtaka Rais Mugabe ang’atuke madarakani kwani video hiyo ni ushahidi tosha kuwa amezeeka.

Katika habari nyingine, serikali ya Zimbabwe imetoa taarifa kuwa Rais Mugabe anatarajiwa kwenda mapumziko ya mwezi mmoja huku Makamu wa Rais akitarajiwa kuiongoza nchi.

Katika taarifa hiyo serikali imewataka wananchi kupuuza habari zitakavyoeleza vinginevyo hasa kuhusu afya ya kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 92.

 

Comments

error: Content is protected !!