tmoja2

Video: Sababu alizotoa Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo wakati akitangaza kuzifungia stesheni mbili za Redio.

2239
0
Share:
Share this
tmoja2

Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ametangaza kuvifungia kwa muda usiojulikana vituo viwili vya Redio kurusha matangazo yao.Waziri Nape ametangaza uamuzi huo katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kuzitaja redio hizo kuwa ni Radio 5 FM ya Arusha na Radio Magic FM ya jijini Dar es Salaam,

Amesema redio hizo kwa nyakati tofauti na katika vipindi vyao tofauti walitangaza habari zilizokuwa na uchochezi ambazo zinaweza kuvuruga amani ya nchi kwa kukiuka masharti ya kanuni ya 5 (a, b, c na d) , kanuni ya 6 (2a, b na c) na kanuni ya 218 ya huduma za utangazaji ya mwaka 2005.

Aidha Nape amesema ameilekeza kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) ili kuwahoji wahusika na kisha kushauri adhabu ambazo zitakazofaa dhidi yao.

Comments

error: Content is protected !!