tmoja2

Video: Sakata la Misaada Kagera, hii ndiyo ilikuwa kauli ya Rais Magufuli

3272
0
Share:
Share this
tmoja2

Kuanzia mwishoni wa juma kumekua na minong’ono kwenye mitandao ya kijamii baada ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu kueleza kiasi cha michango iliyotokana na tetemeko la ardhi kilichokusanywa hadi sasa.

Akizungumza na waandishi wa habari, mkuu wa mkoa alisema kuwa hadi sasa serikali imekusanya kiasi cha shilingi bilioni 5.4, pamoja na vifaa vyenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 2.2 vimekusanywa na kupelekwa kusaidia ujenzi katika majengo ya taasisi za serikali.

Akitolea ufafanuzi wa matumizi ya michango hiyo iliyochangwa, mkuu wa mkoa wa Kagera alisema kuwa itaelekezwa kwenye kujenga na kukarabati miundombinu ya serikali na hivyo kuwataka wakazi wa Kagera walioathiriwa na tetemeko kujijengea nyumba wao wenyewe kwa ni kwa sasa kipaumbele cha serikali ni kuhakikisha kunakuwepo na miundombinu na taasisi za serikali zinakarabatiwa.

Kauli hii imezua maswali mengi huku watu wengi wakihoji kwanini serikali haikusema tangu awali kuwa fedha hizo zilizokuwa zikikusanywa hazitatumika na wananchi? Watumiaji wa mitandao wameeleza kuwa, serikali ilikuwa ikichangisha fedha kwa ajili ya kuwasaidia wa athirika wa tetemeko na si kujenga miundombinu.

Lakini kingine pia walichohoji ni kuwa, wananchi wanalipa kodi, hivyo ni wajibu wa serikali kukarabati miundombinu bila kutegemea michango ya wananchi. Haiwezekani wananchi walipe kodi bado wachangishwe na fedha za kukarabati miundombinu.

Hapa chini ni baadhi ya yaliyozungumzwa mitandaoni jana kuhusu michango ya waathirika wa tetemeko.

Hapa chini ni video ya Rais Dkt Magufuli alipokuwa akizungumzia kuhusu tetemeko la ardhi na mipango ya serikali.

Mpaka sasa Ofisi ya Waziri Mkuu kitengo cha maafa ambacho ndicho kilikuwa kikiratibu zoezi zima la misaada, bado hakijatoa taarifa yoyote.

Comments

error: Content is protected !!