Video: Viongozi wa juu wa kiupelelezi Marekani wakitoa ushahidi wa Urusi kuingilia uchaguzi

376
0
Share:
Share this
CMTL Group

Tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa Marekani Novemba 8 mwaka jana kumekuwa na shutuma nyingi kuhusu Urusi kuingilia uchaguzi wa nchi hiyo na kumwezesha Rais Mteule Donald Trump kushinda baada ya kumbwaga mpinzania wake wa karibu Hillary Clinton.

Licha ya kuwa Urusi imepinga tuhuma zote zilizotolewa kuhusu kuhusika kwake kwa namna yoyote katika uchaguzi mkuu wa Marekani, Rais Barack Obama alikwenda mbali na kuwafukuza wanadiplomasia 35 wa Urusi kwa tuhuma za kuhusika na udukuzi huku akifunga majengo ya taasisi mbili za kiitelijensia za Urusi.

Ripoti ya hivi karibuni kutoka kwa viongozi wa Shirika la Kijasusi la Marekani imethibitisha kuwa Rais Putin wa Urusi binafsi aliagiza udukuzi ufanyike kwa Hillary Clinton ili kumfanya apoteze uhalali kwa wananchi na kumsaidia Trump kushinda.

Hapa chini ni video ya viongozi wa taasisi za juu za kiupelelezi nchini Marekani wakitoa ushahidi kuhusu Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani.

Comments

error: Content is protected !!